700- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliitaja siku ya ijumaa na akasema:

“Ndani yake kuna saa ambayo hakutani nayo mja muislamu ambapo amesimama anaswali na kumuomba Allaah kitu isipokuwa humpa nacho.”

Akaashiria kwa mkono wake kwamba ni [muda] mfupi.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim, an-Nasaa´iy na Ibn Maajah.

Kuhusiana na kuanisha saa hiyo, kumepokelewa juu yake Hadiyth nyingi ambazo ni Swahiyh. Wanachuoni wametofautiana juu yake tofauti nyingi. Nimezitaja katika kitabu kingine. Hapa nitataja tu baadhi ya maoni yanayothibitisha baadhi ya maoni.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/438)
  • Imechapishwa: 13/01/2018