18. Du´aa za kuinuka kutoka kwenye Rukuu´

  Download

38-

سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ

“Allaah amemsikia mwenye kumhimidi.”[1]

39-

رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ، حَمْداً كَثيراً طَيِّباً مُبارَكاً فِيهِ

“Ee Mola wetu, sifa zote njema ni Zako, sifa nyingi, nzuri na zilizobarikiwa ndani yake.”[2]

40-

ربَّنا ولك الحمدُ مِلْءَ السَّمواتِ ومِلْءَ الأرضِ ومِلْءَ ما شِئْتَ مِن شيءٍ بعدُ أهلَ الثَّناءِ والمجدِ أحقُّ ما قال العبدُ وكلُّنا لك عبدٌ لا مانعَ لِما أعطَيْتَ ولا مُعطيَ لِما منَعْتَ ولا ينفَعُ ذا الجَدِّ منك الجَدُّ

“Himdi zilizojaa mbingu, ardhi na vilivyomo ndani yake na vinginevyo vyote vile utakavyo baada yake. Wewe ni mstahiki wa sifa na utukufu, ni ukweli yale yaliyosemwa na mja, na sisi wote Kwako ni waja. Ee Allaah! Hapana awezaye kukizuia kile Ulichokitoa na hapana awezaye kukitoa kile Ulichokizuia na wala haumnufaishi mwenye utajiri, kwani Kwako Wewe ndiko kunatoka utajiri.”[3]

[1] al-Bukhaariy pamoja na “al-Fath” (796).

[2] al-Bukhaariy pamoja na “al-Fath” (796).

[3] Muslim (477).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 30/09/2018