18. Du´aa wakati wa kukutana na adui na mtawala


103- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anapokuwa na khofu kwa mtu anasema:

اللهُمَّ إِنَّا نَجْعَلُكَ في نُحورهم وَنَعُوذُ بك منْ شرورهم

“Ee Allaah! Hakika sisi tunakujaalia kwenye vifua vyao na tunajilinda Kwako kutokana na shari yao.”

104- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema wakati anaposimama mbele ya adui:

اللهُمَّ أَنْتَ عضُدِي وَأَنْتَ ناصرِي بكَ أَحُولُ وَبكَ أَصول وَبك أُقاتلُ

“Ee Allaah! Wewe ndiye msaidizi wangu na Wewe ndiye mnusura wangu. Ninazunguka kwa sababu Yako. Ninashambulia kwa sababu Yako na ninapigana kwa sababu Yako.”

105- ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

حَسْبُنَا اللّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ

“Allaah Anatutosheleza. Naye ni Mbora wa kutegemewa.”

Ibraahiym alisema hivi wakati alipokuwa ametupwa ndani ya moto na Muhammad alisema hivi wakati alipoambiwa:

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُواْ لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَاناً

”Wale ambao waliambiwa na watu: “Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan.” (Aal ´Imraan:173)

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 21/03/2017