18. Dhana mbovu walionayo makhurafi wengi kwa wale wanaodaiwa kuwa ni mawalii wa Allaah

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Kisha mambo yakawa kwa wengi wenye kudai elimu na kwamba yeye ni katika waongofu wa viumbe na wenye kuilinda Shari´ah juu ya kwamba mawalii ni lazima kwao kutowafuata Mitume, na yule mwenye kuwafuata [Mitume] sio katika wao [mawalii]. Isitoshe ni lazima kuacha Jihaad, na yule mwenye kupigana Jihaad sio katika wao [mawalii]. Vilevile ni lazima kuacha imani na kumcha Allaah, na yule mwenye kushikamana na imani na kumcha Allaah basi si katika wao [mawalii hao]. Ee Mola Wetu! Tunakuomba msamaha na afya. Hakika Wewe ni mwingi wa kusikia du´aa.

MAELEZO

Akitoka katika Shari´ah wao wanamwita kuwa ni mtambuzi, kwamba amefika kwa Allaah na kuwa hana haja tena ya kumfata Mtume kwa sababu anapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah. Wanasema kuwa sisi tunaichukua dini yetu kutoka kwa mfu na kutoka kwa mfu mwingine – wakimaanisha cheni za wapokezi wa Hadiyth – na kwamba wao wanaichukua dini yao kutoka kwa Aliye hai ambaye hafi. Wanadai kuwa wanapokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah. Wao wanaonelea kuwa mwenye kuchukua kutoka kwa Mitume sio katika mawalii. Kwa mujibu wao mtu hawi walii isipokuwa mpaka atoke nje ya utiifu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Watu wengi waliokuja nyuma hii leo wanaonelea kuwa mtu hawi walii mpaka kujengwe juu ya kaburi lake banda au msikiti. Kuhusiana na yule ambaye amezikwa kwa mujibu wa Sunnah na hakukujengwa kitu juu ya kaburi lake, mtu kama huyu wanaonelea kuwa sio walii hata kama atakuwa ni katika watu bora. Jengine ni kwamba wanaona kuwa walii anakuwa na staili maalum na huku amevaa kilemba na nguo maalum. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) anasema:

“Mawalii wa Allaah hawana alama maalum yenye kuwatofautisha na wengine. Mawalii wa Allaah wanakuwa kama watu wengine wa kawaida. Hawawi wenye kujulikana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huenda mwenye nywele matifutifu anayefukuzwa milangoni lau atamuapia Allaah [amfanyie jambo fulani] angelimfanyia”.”

Hizi ndio sifa za mawalii wa Allaah ya kwamba hawajionyeshi. Kinyume chake wanafanya bidii kubwa kujificha wasijulikane kwa ajili ya kumtakasia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hivyo sifa za mawalii wa Allaah ni hizi zifuatazo:

1 – Ni wenye kujishusha chini.

2 – Ni wenye kujificha na kutojionyesha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 19/05/2021