Ya pili: Mwaname kutokuwa na hedhi yenye kujulikana kabla ya kupata damu ya ugonjwa kwa njia ya kwamba damu yake ya ugonjwa inaendelea kuanzia pale anapopata damu yake ya kwanza. Mwanamk

e huyu anatakiwa kupambanua kati ya ile damu ya kwanza na ya pili. Hedhi yake ni ile nyeusi, nzito na yenye kunuka. Katika hali hii hapa kunatumika hukumu za hedhi. Ile nyingine yote ni damu ya ugonjwa ambayo ina hukumu zake.

Mfano wa hilo mwanamke anapata damu kwa mara ya kwanza na haikatiki. Hata hivyo damu yake zile siku kumi za mwanzo ni nyeusi na siku zilizosalia za mwezi ni nyekundu, nzito zile siku kumi za mwanzo na khafifu siku zilizosalia za mwezi au ni yenye kunuka zile siku kumi za mwanzo na siku zilizosalia za mwezi sio yenye kutoa harufu. Katika hali hii ana hedhi pale ambapo damu ni nyeusi katika mfano wa kwanza, nzito katika mfano wa pili na yenye kunuka katika mfano wa tatu. Nyingine yote ni damu ya ugonjwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Faatwimah bint Abiy Hubaysh:

“Ikiwa ni damu ya hedhi, ni nyeusi na inajulikana. Ikiwa ni hivyo basi usiswali. Na ikiwa ni nyingine tawadha na uswali. Huo ni mshipa tu.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na an-Nasaa´iy. Ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn Hibbaan na al-Haakim. Hata kama katika mlolongo wa wapokezi na matini yake inahitajia kuangaliwa vizuri wanachuoni wameitendea kazi. Ni bora kwake kwenda kwa mujibu wayo badala ya kuangalia hali za wanawake wengi.

[1] Abu Daawuud (286), an-Nasaa´iy (216) na (363) na al-Haakim (1/174). Ibn Haajar amesema katika ”at-Talkhiys: ”Iko kwa masharti ya Muslim.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016