18. Dalili ya kumi na sita kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe


16- Nilimsomea Abul-Mudhwaffar bin Hamdiy: Muhammad bin Muhammad bin al-Husayn amekukhabarisheni: Ahmad bin Thaabit ametuhadithia: al-Qaasim bin Ja´far ametuhadithia: Muhammad bin Ahmad bin ´Amr ametuhadithia: Sulaymaan bin al-Ash´ath ametuhadithia: Muhammad bin Bashshaar ametuhadithia: Wahb bin Jariyr ametuhadithia: Baba yangu amenihathia: Nimemsikia Muhammad bin Ishaaq akielezea kutoka kwa Ya´quub bin ´Utbah, kutoka kwa Jubayr bin Muhammad bin Jubayr bin Mutw´im, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake aliyesema:

“Kuna mbedui alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Ee Mtume wa Allaah! Nafsi zinaangamia, familia zinahisi njaa na mali zinaangamia. Tuombee kwa Mola wako atunyeshelezee. Sisi tunamuomba Allaah kupitia kwako na kupitia Allaah kwako.” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu!  Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu!”Akaendelea kusema hivo mpaka hilo likatambulika nyusoni mwa Maswahabah zake. Kisha akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Maangamivu ni yako! Allaah haombwi mbele ya kiumbe Wake yeyote. Maangamivu ni yako! Unamjua ni nani Allaah? Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake na ´Arshi Yake iko juu ya mbingu.”[1]

[1] Abu Daawuud (4726) na at-Twabaraaniy katika ”al-Mu´jam al-Kabiyr” (1547).  Ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (1017). adh-Dhahabiy amesema:

“Hadiyth hii ni geni sana. Ibn Ishaaq ni hoja inapokuja katika wasifu maadamu ataeleza ni nani amepokea kutoka kwake. Hata hivyo wakati mwingine anaweza kupokea mambo yenye kupingwa na ya ajabu. Allaah ndiye mjuzi zaidi kama kweli Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema maneno haya au hakusema.

Kuhusiana na Hadiyth hizi, sisi tunaamini zile zilizosihi na zile Salaf walizoafikiana juu ya kuzipitisha na kuzikubali. Kuhusu zile Hadiyth ambazo wanachuoni wametia dosari cheni ya wapokezi wake au wanachuoni wametofautiana juu ya tafsiri zake, sisi tunazipokea katika jumla na kubainisha hali yazo. Nimetaja Hadiyth hii kwa sababu inatiliwa nguvu na yale yaliyopokelewa kwa njia nyingi juu ya kwamba Allaah (Ta´ala) Yuko juu ya ´Arshi pamoja na yale yanayoafikiana na Aayah za Qur-aan.” (al-´Uluww, uk. 39)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 96
  • Imechapishwa: 02/06/2018