Allaah (Ta´ala) amesema:

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ

Na pindi watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi ni Niko karibu; Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.”[1]

Hapa Allaah (´Azza wa Jall) anathibitisha ukaribu Wake kwa waja Wake. Mungu mnayemuabudu yuko karibu nanyi na ni mwenye kuwatambua. Hakuna chochote katika mambo yenu kinachofichikana Naye. Ni wajibu kwenu kulitambua hilo na kumuabudu vile ipasavyo na kumuomba. Mkimuomba anakuitikieni maombi yenu akiona kuna kheri katika yale myaombao. Hapa bila ya shaka kuna maelezo juu ya kwamba Allaah yuko karibu na waja Wake, anaitikia du´aa zao na kuwahimiza nazo. Tukimuomba anatuitikia. Amesema (Ta´ala):

فَلْيَسْتَجِيبُوا لِي وَلْيُؤْمِنُوا بِي لَعَلَّهُمْ يَرْشُدُونَ

Basi waniitikie Mimi na waniamini Mimi ili wapate kuongoka.”[2]

Anatuitikia kwa sharti tumuitikie pale Yeye (´Azza wa Jall) anapotuita; tusiache kufanya maamrisho Yake ambayo tunaweza kuyatekeleza au kufanya kitu cha madhambi hali ya kujua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa mja anapomuomba Allaah (´Azza wa Jall) basi ni lazima apate moja katika mambo matatu:

1- Amuitikie pale (´Azza wa Jall) atapoona ni chenye kheri na yeye.

2- Amuepushe na shari kiwango chake.

3- Amuwekee maombi yake kwa ajili ya siku ya Qiyaamah.

Pindi mja anapomuomba Allaah basi anapata moja katika mambo haya matatu[3].

[1] 02:186

[2] 02:186

[3] al-Bayhaqiy (3968). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” (522).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 29-32
  • Imechapishwa: 02/06/2017