Pindi Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy anaposema fulani ni “Hizbiy”


Miongoni mwa watu leo walio na uoni wa mbali na ujuzi kuhusu makundi na matawi ya makundi, ni ndugu Shaykh Rabiy´ bin Haadiy (Hafidhwahu Allaah). Wakati Shaykh Rabiy´ anaposema kuwa mtu fulani ni “Hizbiy”, itakuja kufichuka siku moja kweli kwamba ni Hizbiy. Mtakuja kukumbuka hilo. Inahusiana tu na kwamba mtu huyo mwanzoni jambo lake litakuwa halijulikani na kwa ajili hiyo ndio maana hataki hali yake iweze kujulikana. Hata hivyo hili hubadilika wakati anapopata nguvu kidogo na akawa na baadhi ya wafuasi na wakati huo huo anaonelea kuwa haathiriki kwa kuzungumziwa vibaya. Kwa ajili hiyo ndio maana nashauri mtu kusoma vitabu vyake (Hafidhwahu Allaah) na kustafidi navyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mkanda ”al-As-ilah as-Sunniyyah li ´Allaamah ad-Diyaar al-Yamaniyyah - As-ilah Shabaab at-Twaaif”
  • Imechapishwa: 03/04/2017