177. Inafaa kwa mwanamke aliye katika eda kujipaka mafuta yanayonukia vizuri?


Swali 177: Je, inafaa kwa mwanamke aliye ndani ya eda ya kufiwa na mume wake kuosha kichwa chake? Je, inafaa kwake kujipaka mafuta yenye kunukia vizuri na kujitia krimu[1]?

Jibu: Hapana vibaya kwa mwanamke aliye katika eda kuosha kichwa chake na mwili wake mzima kwa kile atachokitaka ni mamoja kiwe mkunazi au vyenginevyo visivyonukia vizuri. Kuhusu kujipaka mafuta au kujiosha kwa kitu kilicho na harufu ya manukato haifai. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkataza mwanamke aliye ndani ya eda kujitia manukato isipokuwa uvumba kidogo wakati anapojiosha kutokamana na hedhi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/204-205).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 133
  • Imechapishwa: 08/02/2022