176. Makatazo ya kumposa mwanamke aliye katika eda

Swali 176: Je, inafaa kwa mwanamke anayemkalia eda mume wake kuwaosha watoto wake na kuwatia manukato? Je, inafaa kuposwa ilihali yuko ndani ya eda[1]?

Jibu: Haifai kwa mwanamke ambaye yuko katika eda ya kufiwa na mume wake kujitia manukato. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Lakini hapana vibaya kuwasogelea watoto wake na wageni wake pasi na kuchanganyikana nao katika hayo. Haijuzu kuposwa uposaji wa wazi mpaka pale atakapotoka katika eda. Hapana neno kumwashiria pasi na kumuwekea wazi. Amesema (Ta´ala):

وَلَا جُنَاحَ عَلَيْكُمْ فِيمَا عَرَّضْتُم بِهِ مِنْ خِطْبَةِ النِّسَاءِ

“Wala si dhambi juu yenu katika ambayo mmedokezea ya kuposa wanawake hao.”[2]

Ameruhusu (Subhaanah) kumwashiria na hakuruhusu kumuwekea wazi. Yeye (Subhaanah) ana hekima kuu juu ya jambo hilo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/203-204).

[2] 02:235

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 132
  • Imechapishwa: 07/02/2022