175. Eda ya mwanamke aliyezaa kwa upasuaji baada ya mume wake kufariki


Swali 175: Kuna mwanamme yeye na mke wake walipata ajali ya barabarani. Mke wake alikuwa na ujauzito wa miezi minane ambapo mwanamme akaaga dunia na mwanamke akanusurika. Baada ya kumfikisha hospitali madaktari wakaamua kumfanyia upasuaji ya kutoa kile kijusi. Alitolewa nje na alikuwa ni mtoto wa kike ambaye amefariki. Je, mwanamke huyu atatakiwa kukaa eda kama wengine[1]?

Jibu: Kujengea yale mliyoyataja eda ya mwanamke huyo mlengwa itakuwa imemalizika. Kipindi chake cha kumkalia eda mume na kuacha kujipamba kimemalizika kwa kule kujifungua. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/221).

[2] 65:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 07/02/2022