174. Mwanamke ambaye amefiwa na mumewe siku zake zinakamilika kwa masiku au kwa miezi?

Swali 174: Kuhusu mwanamke ambaye amefiwa na mumewe siku zake zinakamilika kwa masiku au kwa miezi? Ni mamoja mwezi umetimia kwa siku 20 au siku 30[1]?

Jibu: Eda ya mwanamke aliyefiwa ni miezi minne na siku kumi. Hapa ni pale ambapo si mwenye ujauzito. Haya ni kwa maafikiano ya waislamu. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَالَّذِينَ يُتَوَفَّوْنَ مِنكُمْ وَيَذَرُونَ أَزْوَاجًا يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ أَرْبَعَةَ أَشْهُرٍ وَعَشْرًا

“Na wale wanaofishwa miongoni mwenu na wakaacha wake, hao wake wangojee peke yao [eda ya] miezi minne na siku kumi.”[2]

Ni siku mia moja na thelathini. Lakini akihifadhi kuwa baadhi ya miezi ni siku 29 basi atakaa eda kwa mujibu wake. Kama mume atakufa mwisho wa Sha´baan na Ramadhaan ikawa siku 29 basi atakaa eda kwa mujibu wake. Vivyo hivyo Shawwaal na Dhul-Qa´adah ikithibiti kuwa kila kimoja ni siku 29 basi atakaa eda kwa mujibu wake. Kuhusu miezi mingine ambayo haikuthibiti katika mahakama za ki-Shari´ah kuwa ni pungufu, basi atazingatia kila mwezi ni 30 mpaka pale atapokamilisha eda yake.

Kuhusu mjamzito eda yake itamalizika kwa kujifungua. Ni mamoja ametalikiwa au amefiwa na mumewe. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَأُولَاتُ الْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ

“Na wenye mimba muda wao [wa eda] watakapozaa mimba zao.”[3]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/219-220).

[2] 02:234

[3] 65:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 06/02/2022