171. Mwanamke aliye eda kuzungumza na wanamme

Swali 171: Kuna mwanamke amefiwa na mumewe akiwa bado ni mdogo. Ni yepi yaliyoharamishwa kwake mbali na kujipamba? Je, awapokee wanamme wa kando naye, awasalimie na azungumze nao kama mfano wa mwanamke ambaye hakukaa eda kwa hoja kwamba hakuna yaliyoharamishwa kwake isipokuwa mfano wa yale yaliyoharamishwa kwake anapokuwa hakukaa eda? Angalizo ni kwamba anaishi katika jamii ambayo haioni vibaya kusalimiana kwa kupeana mikono. Tunaomba kuwekewa wazi hukumu na vigezo[1]?

Jibu: Ni lazima kwake kukaa eda kwa muda wa miezi minne na siku kumi. Ni mamoja bado mdogo au mtumzima. Vilevile inafaa kwake kuzungumza na wanamme katika jamaa zake au wengineo haja ikipelekea kufanya hivo. Sambamba na hilo anapaswa kujisitiri, kutokaa chemba na kutolegeza mayai. Haifai kwake kusalimiana kwa kupeana mikono na wanamme wasiokuwa Mahaarim zake.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/206-207).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 128
  • Imechapishwa: 29/01/2022