170. Anataka kwenda kukaa eda nyumbani kwa mwanae


Swali 170: Baba yangu amefariki na mama yake ni kikongwe na yuko katika eda. Ametaka kutoka nje na kwenda kwa mmoja katika wasichana zake. Kwa sababu kikongwe huyo ni mgonjwa na anapokaa nyumbani anachoka na ndio maana anataka kwenda kwa mmoja katika wasichana zake. Kwa sababu kukaa nyumbani kunamchosha sana. Je, inafaa kwake kwenda kwa mmoja katika wasichana zake ilihali yuko ndani ya eda[1]?

Jibu: Inafaa kwake kufanya hivo akihitaji kufanya hivo na ikiwa sio rahisi kwa msichana wake kuja nyumbani kwake na ikiwa sio rahisi kupata mtu wa kumhudumia nyumbani. Allaah (Subhaanah) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/205-207).

[2] 64:16

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 01/02/2022