17- Wanawateua viongozi juu ya wanachama wao katika kila wilaya au mji, kutokana na haja. Mara nyingi viongozi hawa wanakuwa ni vijana walioghurika na uongozi wao wenyewe. Uongozi unawaacha uwalee watu kutokana na vidhibiti vya mfumo. Baada ya hapo wanachukua viapo vya usikivu na utiifu ambavyo havikutolewa na watu isipokuwa baada ya kupitia hatua kadhaa katika kipindi kirefu. Viapo hivyo vinakuwa na dibaji mbalimbali, makubaliano na mikataba. Haya nimeyasikia kwa watu waliokuwa nao kisha wakaachana nao kwa ajili ya mfumo wa Salaf ulio wazi na salama. Ni siri ngapi zinazopatikana katika viapo hivyo vya ki-Bid´ah! Baadhi yao walifichuka kama wale walipuaji ar-Riyaadh. Hata kama mtandao wao bado utaendelea kufanya kazi basi usitarajie jengine zaidi ya ajali na matukio makubwa makubwa.[1]

[1] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 23
  • Imechapishwa: 25/03/2017