Kuna tofauti kati ya Tawalliy (التولي) na Muwaalaah (الموالاة). Kufanya Tawalliy na makafiri ni kuritadi. Kuhusu kufanya Muwaalaah na wao, kwa msemo mwingine kuwapenda, kutangamana nao na kuwa na urafiki nao ni dhambi kubwa. Msingi wa Tawalliy ni kuwa na mapenzi ndani ya moyo. Mapenzi haya baadaye yanazalisha kuwasapoti na kuwasaidia. Kile kitendo chake cha kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu, ni mamoja iwe kwa mali, silaha au maoni, ni dalili tosha ya yeye kuwa na Tawalliy kwa makafiri na kwamba anawapenda, jambo ambalo ni kuritadi kutokana na dalili ya Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ

“Enyi mlioamini! Msiwafanye mayahudi na manaswara kuwa ni marafiki… “

Bi maana usifanye nao Tawalliy.

بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ

“…. wao kwa wao ni marafiki.”

Makafiri ni wapenzi wao kwa wao.

وَمَن يَتَوَلَّهُم

“Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao… “

Bi maana makafiri.

مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ

“… katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao.”

Bi maana muislamu ambaye atafanya Tawalliy na makafiri basi yeye ni katika wao. Ni kafiri kama wao.

وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ

“Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah haongoi watu madhalimu.”

Kwa hivyo kuwasapoti na kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni kuritadi. Kwa sababu huku ni kufanya Tawalliy na makafiri. Kufanya Tawalliy na makafiri ni kuritadi na kutoka nje ya Uislamu kwa dalili ya Qur-aan.

[1] 05:51

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tabswiyr-ul-Anaam bisharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 47
  • Imechapishwa: 15/04/2023