17. Sunnah na maana yake mbalimbali

Utiifu umegawanyika sampuli mbili:

1 – Mambo ya wajibu.

2 – Mambo yaliyopendekezwa.

Neno “Sunnah” linaweza kuwa na maana nyingi:

1 – Yale yaliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah na ´ibaadah.

2 – ´Aqiydah. Ndio maana vitabu vya ´Aqiydah vinaitwa “as-Sunnah”, kama mfano wa “as-Sunnah” cha ´Abdullaah bin Imaam Ahmad na “as-Sunnah” cha Ibn Abiy ´Aaswim. Vinaitwa pia vitabu vya “al-Iymaan”, kama mfano wa “al-Iymaan” cha Ibn Mandah.

Kuhusu Sunnah kwa mujibu wa Muhaddithuun ni yale yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika maneno, vitendo, kulipitisha jambo au sifa.

Sunnah kwa maana hii yenye kuenea inatofautiana. Ipo Sunnah ambayo ni ya lazima, ipo Sunnah ambayo imependekezwa. Sunnah iliyopendekezwa iko ambayo imekokotezwa zaidi, Sunnah ambayo haiko hivo. Mfano wa Sunnah hiyo ni kama zile swalah zilizopendekezwa zinazoswaliwa kwa mnasaba wa zile swalah za faradhi  (الرواتب), Witr na Dhuhaa. Zipo Sunnah zengine ambazo zimefungamanishwa na nyakati, kama mfano wa Rak´ah mbili wakati wa kuingia msikitini na Dhuhaa. Vilevile zipo Sunnah ambazo hazikufungamanishwa katika nyakati zote mbali na zile nyakati mtu amekatazwa kuswali ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 07/07/2021