17. Sifa za mawalii wa Allaah katika Aayah tatu

Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimhu Allaah) amesema:

Na Aayah katika Suurah “al-Maaidah” ambayo ni maneno Yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ

Aayah nyingine katika Suurah “Yuusuf” ambayo ni maneno Yake:”Enyi mlioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu kutoka dini yake, basi punde tu Allaah ataleta watu [badala yao] atakaowapenda nao watampenda.” (05:54)

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa na uchaji.” (10:62-63)

MAELEZO

Na Aayah katika Suurah “al-Maaidah” – Hizi ndio sifa za mawalii wa Allaah. Wao wanampenda Allaah na Allaah Naye anawapenda. Wanakuwa:

أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ

“… wanyenyekevu kwa waumini, wenye nguvu juu ya makafiri.” (05:54)

Bi maana wanawapenda na ni wenye mapenzi kwa waumini na wakati huohuo wanawachukia na ni wenye kujitenga mbali na washirikina:

يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ

“… wanapambana katika njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama ya [yeyote] anayelaumu.” (05:54)

Sifa hizi nne ndio sifa za mawalii wa Allaah.

Kuhusiana na wale wenye kuwaamrisha watu kuabudia asiyekuwa Allaah, wanawaomba wafu walio ndani ya makaburi, mambo yanayokwenda kinyume na hali ya kawaida wanaita kuwa ni “makarama ya Allaah”, hizi ni sifa za maadui wa Allaah.

Aayah nyingine katika Suurah “Yuusuf” – Chukua katika Aayah hizi tatu sifa za mawalii wa Allaah:

1 – Aayah katika Suurah “Aal ´Imraaan”.

2 – Aayah katika Suurah “al-Maaidah”.

3 – Aayah katika Suurah “Yuusuf”.

Katika Aayah hizi kuna sifa za mawalii wa Allaah. Mwenye kusifika na sifa hizi, basi huyo ndiye walii wa Allaah. Na yule mwenye kusifika na sifa kinyume na hizi, basi huyo ni walii wa shaytwaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sittah, uk. 37
  • Imechapishwa: 19/05/2021