17. Ndio maana magharibi hawawezi kupambana na ugaidi

Kuhusu kupambana na ugaidi katika nchi za kikafiri, ni jambo limejengwa juu ya kanuni zao wenyewe. Hata kama kanuni zao zitaondosha madhara fulani ni lazima ziwe kombo. Hivyo ugaidi utaendelea tu kuzidi na kuenea katika miji yao. Utaendelea kuwasibu mara kwa mara, mchana kweupee, kwa kuwa hawatarajii utukufu wa Allaah vile anavyostahiki kutukuzwa – ilihali Yeye ndiye kawaumba hatua kwa hatua!

Jambo lenye kusitikisha sana ni kwamba miji mingi ya Kiislamu imeifuata kichwa mchunga miji ya kikafiri na kuhukumu kwa sheria za binaadamu katika mambo ambayo haijuzu kuhukumiwa nayo. Si vyenginevyo bali ni wajibu kuhukumu kwa Shari´ah ya Allaah iliyo safi na kamilifu. Kwa kuwa miji ya Kiislamu inajinasibisha na Uislamu na inajifakharisha nao katika khabari na kauli mbiu zao. Baadhi ya miji ya Kiislamu imeondoa Shari´ah zilizowekwa na kuchagua kuwafuata kichwa mchunga watu katika viongozi wa kikafiri wakanamungu waasi. Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutakorejea!

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 24
  • Imechapishwa: 14/04/2017