Miongoni mwa misingi ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kusadikisha karama za mawalii. Ni mambo yasiyokuwa ya kawaida ambayo Allaah wakati mwingine huyapitisha kupitia mikono ya baadhi ya watu ili kuwaheshimisha. Hilo limefahamishwa na Qur-aan na Sunnah. Mu´tazilah na Jahmiyyah wamepinga kutokea kwa karama. Huku ni kupinga kitu cha uhalisia na kinachojulikana.

Lakini hata hivyo tunapaswa kujua kuwa hii leo kuna watu wamepotea katika maudhui haya ya kuhusu karama na wakapetuka mipaka kiasi cha kwamba wakafikia kuingiza ndani yake yasiyokuwemo katika uchawi, matendo ya kichawi, mashaytwaan na madajali.

Kuna tofauti ya wazi kati ya karama na uchawi. Karama ni yale hupitika kwenye mikono ya waja wa Allaah walio wema. Uchawi ni yale hupitika kwenye mikono ya wachawi, makafiri na wakanamungu kwa lengo la kuwapotosha viumbe na kuwalia pesa zao. Karama inatokana na ni utiifu. Uchawi unatokana na ukafiri na maasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 37-38
  • Imechapishwa: 13/05/2022