Aliyepewa msiba anatakiwa kutambua kuwa mahuzuniko hayaurudishi msiba. Bali yanaufanya tu kuwa mbaya zaidi. Uhakika wa mambo ni kuwa msiba unazidi. Msibiwaji anatakiwa kujua kuwa mahuzuniko yanamfurahisha adui, yanamuudhi rafiki, yanamkasirisha Mola, yanamfurahisha shaytwaan, yanaharibu thawabu zake na kumdhoofisha yeye mwenyewe.

Lau atakuwa na subira na kutarajia malipo kwa Allaah anamdhalilisha shaytwaan wake, anamridhisha Mola wake, anamfurahisha rafiki yake na anamuudhi adui wake. Haya ndio yamethibiti katika dini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ee Allaah! Ninakuomba uthabiti katika jambo.” at-Tirmidhiy na an-Nasaa’iy.

Huu ndio ukamilifu mkubwa na sio kujipiga kwenye mashafu, kuchana nguo, kuomba umauti na kuhisi hasira juu ya Qadar.

Baadhi ya Salaf wamesema:

“Mwerevu hufanya katika ile siku ya kwanza yale mjinga hufanya masiku mengi baada yake. Asiyesubiri kama watukufu husahau kama mifugo.”

Kinachomaanishwa ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yaliyothibiti katika Hadiyth Swahiyh:

“Hakika subira huzingatiwa katika kile kipindi cha kwanza.”

al-Ash´ath bin Qays amesema:

“Ima utasubiri na huku ukitarajia malipo au utasahau kama mfugo.”

Mwenye kusibiwa anatakiwa kujua kuwa utamu na ile furaha inayopatikana kwa kuwa na subira na matarajio ya thawabu wakati wa msiba ni jambo kubwa kabisa zaidi kuliko kile alichokuwa nacho endapo asingelipatwa na msiba huo. Inatosheleza kwake kupata nyumba ya Mshukuriwaji Peponi kwa sababu amemshukuru Mola wake na amesema “Sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea” wakati wa msiba. Ndio maana anatakiwa kufikiria ni msiba upi ulio mkubwa; msiba wa hapa duniani kwa maana ya kwamba mtu kumkosa kipenzi chake au msiba wa huko Aakhirah kwa maana ya kwamba mtu kukosa nyumba ya Mshukuriwaji katika Pepo ya milele?

Mwenye kuhuzunika na mtu mwenye msiba anatakiwa kujua kuwa vyovyote huzuni wake utavyokuwa, kutokuwa kwake na subira ni jambo lisilosifiwa wala kulipwa thawabu pamoja na kuzingatia ya kwamba hana khiyari ya jengine. Kwa sababu katika hali hii amejisalimisha na subira kwa hali ya kutopenda. Yahyaa bin Mu´aadh amesema:

“Ee mwanaadamu! Kwa nini unasikitika kwa ulichokikosa ambacho hutokipata tena na kwa nini unafurahikia kitu ambacho kifo haitokiacha?”

Pindi msikitikaji anapojua kuwa kusikitika hakumrudishii alichokikosa na ukiongezea juu ya hilo jambo hilo linamfurahisha adui, mtu anaweza kuuliza ni uelewa upi mtu anatakiwa kuwa nao endapo mtu atafikiria matokeo na kwamba misiba ni lazima itokee sasa au kwa hapo baadae. Baada ya hapo mtu ajiadae nayo.

Kulikuwepo mwanamke mwema Baswrah ambaye alikuwa akipatwa na misiba bila ya kusikitika. Alipoulizwa juu ya hilo akasema:

“Sipatwi na msiba wowote isipokuwa hufikiria Moto. Hivyo basi msiba huo kwenye macho yangu huwa mdogo kuliko nzi.”

Kingine kinachomliwaza mja ni maneno ya baadhi ya wenye hekima:

“Kila Mtume na kila mwenye busara, mjuzi na mwanachuoni amekufa. Hivyo usisikitike.”

Baadhi ya Salaf waliombwa kama wanaweza kutoa mawaidha wakasema:

“Tazama watu wanaoeshi katika zama zako mpaka wakati wa Aadam. Kuna unayemwona anakapua kwa macho?”

Hivyo wakaambiwa:

“Inatosha.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 28
  • Imechapishwa: 14/10/2016