17- Madhambi yanapelekea katika udhalilifu


Madhambi bila shaka yanapelekea katika udhalilifu. Utukufu wote unapatikana katika kumtii Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَن كَانَ يُرِيدُ الْعِزَّةَ فَلِلَّـهِ الْعِزَّةُ جَمِيعًا

“Yeyote anayetaka utukufu, basi [atambue kuwa] utukufu wote uko kwa Allaah.”[1]

Bi maana mtu autafute katika kumtii Allaah. Kwani hawezi kuupata isipokuwa kwa kumtii Allaah. Kuna baadhi ya Salaf walikuwa wakisema:

اللهم أعزَّنِي بِطاعَتِك , ولا تُذِلَّني بمعصيتك

“Ee Allaah! Nitukuze kwa kukutii na wala usinifedheheshe kwa kukuasi.”

al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Hata kama watawapanda nyumbu na farasi wa kazi hakika udhalilifu wa maasi hauziachi nyoyo zao. Hakuna kitu anachomfanya Allaah yule anayemuasi isipokuwa kumdhalilisha.”

[1] 35:10

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 71
  • Imechapishwa: 08/01/2018