123- ´Abdul-´Aziyz bin al-Mukhtaar amepokea kupitia kwa Khaalid al-Hadhdhaa´ kutoka kwa Abu Qulaabah kutoka kwa Abu Asmaa´ kutoka kwa Thawbaan ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kutakuja bendera za rangi nyeusi kutoka upande wa mashariki. Ni kana kwamba nyoyo zao ni kama vipande vya chuma. Atakayesikia kuhusu wao awaendee hata kama atahitajia kutambaa juu ya theluji. Watapofika Dameski wataibomoa jiwe kwa jiwe na kuwaua watoto wa mfalme wake.”

Hadiyth hii imepokelewa na ath-Thawriy na wengineo kutoka kwa Khaalid al-Hadhdhaa´ bila ya nyongeza hii.

Ahmad ameipokea kupitia kwa ´Aliy bin Zayd kutoka kwa Abu Qulaabah. Ibn Maajah na al-Haakim wameipokea kutoka kwa ath-Thawriy. Humo ametajwa vilevile al-Mahdiy.

Ismaa´iyl bin ´Ulayyah alikuwa akiikataa Hadiyth hii. ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal amesema katika “al-´Ilal”:

“Baba yangu alinihadithia ya kwamba kulisemwa kuambiwa Ibn ´Ulayyah ya kwamba al-Hadhdhaa´ ndiye kaipokea Hadiyth hii, lakini Ibn ´Ulayyah akaipuuza kabisa na kuoenela kuwa ni dhaifu. Kunamaanishwa Hadiyth kuhusu bendera za rangi nyeusi ya Khaalid bin al-Hadhdhaa´ kutoka kwa Abu Qulaabah kutoka kwa Ismaa´iyl kutoka kwa Thawbaan.”

Endapo Hadiyth itasihi basi inalenga pale Banul-´Abbaas walipoiteka Dameski na kuingia kwa ´Abdullaah bin ´Aliy bin ´Abdillaah bin ´Abbaas ndani ya mji huo. Kuta zake zilibomolewa na wakaazi wake wa Banu Umayyah na wafuasi wao wakauawa.

124- Junaadah bin Marwaan ameeleza kutoka kwa baba yake aliyesema:

“Nimewasikia wanachuoni wakisema kuwa watu wataokuwa na manufaa makubwa zaidi ya zile bendera zenye rangi nyeusi Shaam ni watu wa Dameski na kwamba watu wataokuwa na manufaa makubwa ya zile bendera zenye rangi ya manjano ni watu wa Hims.”

Hii ni ishara ya yale yaliyotokea kipindi Banul-´Abbaas walipoingia Dameski.

125- Bishr bin Ghunm amesema:

“Dameski itabomolewa jiwe kwa jiwe.”

Haafidhw Abul-Qaasim amesema:

“Huenda anamaanisha wakati ´Abdullaah bin ´Aliy alipobomoa kuta zake pindi alipouteka mji huo.”

126- Mwongo na mzushi ´Abdullaah bin Sayyaar anadai kuwa kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib amemweleza ya kwamba ataingia Dameski na kubomoa msikiti wake jiwe kwa jiwe. Haya ni miongoni mwa ambayo Ibn Sayyaar amemzulia. Imethibiti ya kwamba ´Aliy amekataza kuwatukana watu wa Shaam na waja wema na wachaji watakuwa ni wenye kubadilishana huko Shaam.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 136-140
  • Imechapishwa: 10/02/2017