17. Kichinjwa kinakuwa haramu kwa kuritadi

4- Kuharamika wanyama wa mifugo wanaochinjwa.

Wanyama wa mifugo ni kama ngamia, ng´ombe, kondoo na wanyama wengine ambao ni lazima kuwachinja ili wawe halali kuwala. Ili nyama iwe halali kumeshurutishwa mchinjaji awe muislamu, myahudi au mkristo. Si halali kula nyama iliyochinjwa na mwenye kuritadi, mshirikina, muabudu moto na watu mfano wao. al-Khaazin amesema katika Tafsiyr yake ya Qur-aan:

“Kuna maafikiano juu ya uharamu wa kula nyama iliyochinjwa na waabudu moto na washirikina wengine katika washirikina wa kiarabu, waabudu masanamu na watu wasiokuwa na Kitabu.”

Imaam Ahmad amesema:

“Sijui kama kuna aliyesema kinyume isipokuwa ikiwa kama ni mtu wa Bid´ah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Hukm Taarik-is-Swalaah, uk. 18
  • Imechapishwa: 22/10/2016