17. Katika hali hii hakuna neno mwenye hedhi kusoma Qur-aan

Swali 17: Ni ipi hukumu ya mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kusoma Qur-aan kwa kutazamia na kwa hifdhi katika hali ya dharurah kama akiwa mwanafunzi au mwalimu?

Jibu: Hakuna ubaya kwa mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi kusoma Qur-aan ikiwa kunatokana na haja. Kama mfano mwanamke ambaye ni mwalimu au mwanafunzi wa kike ambaye anarudilia masomo wakati wa usiku au mchana.

Kuhusu kusoma Qur-aan kwa minajili ya kutafuta ujira na thawabu bora ni yeye kutofanya hivo. Kwa sababu wanachuoni wengi wanaona kuwa haifai kwa mwenye hedhi kusoma Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 17
  • Imechapishwa: 26/06/2021