17. Jihaad iliidhinishwa Makkah, ikafaradhishwa al-Madiynah

Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipotulizana al-Madiynah kati ya Answaar na wakachukua jukumu la kumnusuru na kumlinda dhidi ya watu wote, ndipo waarabu wakakusanyika wote dhidi yao na wakawavamia kutoka kila pembe. Allaah alikuwa amewapa idhini waislamu kutoka kwenda katika Jihaad katika Suurah ”al-Hajj” iliyoteremshwa kipindi cha Makkah. Allaah (Ta´ala) amesema:

أُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَاتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ

”Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa kwa kuwa wamedhulumiwa; na hakika Allaah ni Muweza wa kuwanusuru.”[1]

Walipokuwa na nguvu za kutosha al-Madiynah ndipo Allaah akawafaradhishia Jihaad. Allaah (Ta´ala) amesema katika Suurah ”al-Baqarah”:

 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

”Mmefaradhishiwa kupigana vita – nako kunachukiza mno kwenu – na huenda mkalichukia jambo ilihali ni lenyewe kheri kwenu na huenda mkapenda jambo ilihali ni lenyewe shari kwenu.  Allaah anajua na nyinyi hamjui.”[2]

[1] 22:39

[2] 02:216

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 40
  • Imechapishwa: 25/04/2018