17. Hadiyth “Hiyo ndio mirathi ya Muhammad!”

83- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) siku moja alipita karibu na soko la Madiynah akasimama na kusema: “Enyi watu wa sokoni! Kipi kimekufanyeni kushindwa!” Wakasema: “Vipi, ee Abu Hurayrah?” Akasema: “Mirathi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inagawanywa na nyinyi mko hapa. Kwa nini msende na nyinyi mjitwalie fungu lenu?” Wakasema: “Iko wapi?” Akasema: “Msikitini.” Wakatoka matiti. Abu Hurayrah akasimama palepale mpaka waliporudi.” Abu Hurayrah akawaambia: “Mna nini?” Wakasema: “Ee Abu Hurayrah! Tumefika msikitini na tukaingia ndani yake na hatujaona kitu kinachogawanywa.” Abu Hurayrah akawaambia: “Hamkumuona msikitini yeyote?” Wakasema: “Ndio. Tumewaona watu wanaswali, wengine wanasoma Qur-aan, wengine wanadarisishana ya halali na ya haramu.” Ndipo Abu Hurayrah akawaambia: “Ole wenu! Hiyo ndio mirathi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)!”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Nzuri kutoka kwa Swahabah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/143)
  • Imechapishwa: 29/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy