Download

33-

سُبْحانَ رَبِّيَ الْعَظِيمِ

“Ametakasika, Mola wangu, Aliye mtukufu.”[1]

mara tatu[2].

 34-

سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ رَبَّنَا وَبِحَمْدِكَ، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي

“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah Mola wetu, na himdi zote ni Zako. Ee Allaah! Nisamehe.”[3]

35-

سُبُّوُحٌ، قُدُّوسٌ، رَبُّ المَلاَئِكَةِ وَالرُّوحِ

“Mwingi wa kutakaswa, mtakatifu, Mola wa Malaika na roho [Jibriyl].”[4]

36-

اللَّهُمَّ لَكَ رَكَعْتُ، وَبِكَ آمَنْتُ، وَلَكَ أَسْلَمْتُ، خَشَعَ لَكَ سَمْعِي، وَبَصَرِي، وَمُخِّي، وَعَظْمِي، وَعَصَبِي، [وَمَا استَقَلَّتْ بِهِ قَدَمِي

“Ee Allaah! Kwako nimerukuu, Wewe nimekuamini, Kwako nimejisalimisha, umenyenyekea Kwako usikizi wangu, uoni wangu, ubongo wangu, mfupa wangu, hisia zangu na ambacho kimesimama juu ya miguu yangu.”[5]

37-

سُبْحَانَ ذِي الْجَبَرُوتِ، وَالْمَلَكُوتِ، وَالْكِبْرِيَاءِ، وَالْعَظَمَةِ

“Ametakasika Mwenye utawala, ufalme, ukubwa na utukufu.”[6]

[1] al-Bukhaariy pamoja na “al-Fath” (03/03), Muslim ameipokea kwa ufupi mfano wake (769).

[2] Wameipokea watunzi wa Sunan, Ahmad, Abu Daawuud (870), at-Tirmidhiy (262), an-Nasaa´iy (1007), Ibn Maajah (897) na Ahmad (3514). Tazama “Swahiyh at-Tirmidhiy” (01/83).

[3] al-Bukhaariy (794) na Muslim (484).

[4] Muslim (487) na Abu Daawuud (872).

[5] Muslim (771), watunzi wa Sunan wane isipokuwa Ibn Maajah, Abu Daawuud (760) na wengineo.

[6] Abu Daawuud (873), an-Nasaa´iy (1131), Ahmad (23980) kwa cheni ya wapokezi nzuri.

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 30/09/2018