17. Du´aa wakati wa janga, hamu na huzuni

97- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema wakati wa kupatwa na janga:

لا إِله إِلاَّ اللهُ الْعَظِيمُ الْحَلِيمُ لاَ إِله إِلاَّ الله رَبُّ الْعَرْشِ العظيم لاَ إِلهَ إِلاَّ الله ربُّ السَّمواتِ وَرَبُّ الأَرض وَرَبُّ العرش الْكَرِيم

“Hakuna mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, aliye Mtukufu Mpole. Hakuna mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Mola wa ´Arshiy tukufu. Hakuna mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, Mola wa mbingu, Mola wa ardhi na Mola wa ´Arshiy tukufu.”

98- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa linapomuhuzunisha jambo akisema:

يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ برَحْمَتِكَ أَسْتَغِيثُ

“Ee Uliyehai! Ee Msimamizi wa kila kitu! Ninaomba msaada kwa Rahmah Zako.”

99- Abu Bakrah (Radhiya Allaahu ´anhu) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

اللَّهُمَّ رَحْمَتَكَ أَرْجُو فَلاَ تَكِلْني إِلى نفسي طَرْفَةَ عَيْن وَأَصْلِح لِي شَأْنِي كُلَّهُ لا إِلهَ إِلاَّ أَنْتَ

“Ee Allaah! Nataraji Rahmah Zako. Usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa kukapua kwa jicho. Nitengenezee mambo yangu yote. Hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe.”

100- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Asmaa´ bint ´Umays:

”Nisikufunze neno utakalolisema wakati wa janga? [Sema:]

الله الله رَبي لاَ أُشْرِكْ بِهِ شَيئاً

”Ee Allaah! Ee Allaah! Mola Wangu! Sikushirikishi na chochote.”

101- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Dhuun-Nuun aliomba pindi alipokuwa tumboni mwa nyangumi:

لَّا إِلَهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ

“Hapana mola wa haki isipokuwa Wewe! Umetakasika! Hakika nilikuwa katika madhalimu.”

Hakuna Muislamu anayeomba hivyo kwa kitu isipokuwa Allaah Humuitikia.”

102- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mja anayesibiwa na majonzi na huzuni na kusema:

اللهُمَّ إِني عَبْدُكَ وابنُ عَبْدِكَ وابْنُ أَمتِكَ نَاصيتي بيَدِكَ ماضٍ فِيَّ حُكْمُكَ عَدْلٌ فيَّ قَضَاؤُكَ أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيتَ بِهِ نَفْسَكَ أَوْ أَنْزَلْتَهُ في كِتَابِكَ أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحداً مِن خَلْقِكَ أَوِ اسْتَأْثَرْتَ بِه في علم الْغَيْبِ عِنْدَكَ أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ العظيمَ رَبيع قَلْبي ونورَ صَدْرِي وجلاءَ حُزْنِي وَذَهَابَ هَمِّي

“Ee Allaah! Hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako na mtoto wa mjakazi Wako. Utosi wangu uko Mikononi Mwako. Yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako. Hukumu Yako ni adilifu kwangu. Nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako ulilojiita Kwako mwenyewe au uliloliteremsha katika Kitabu Chako au ulilomfundisha yeyote katika viumbe Vyako au ulilolikhusisha Wewe mwenyewe katika Elimu iliyojificha kwako, ujaalie Qur-aan tukufu iwe ni nguvu ya roho yangu na nuru ya kifua changu inayotoa huzuni wangu na kuondoka majonzi yangu”

isipokuwa Allaah Ataondosha majonzi na huzuni wake na kumbadilishia sehemu yake kwa faraja.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 70-72
  • Imechapishwa: 21/03/2017