Damu ya ugonjwa ina hali tatu:

Ya kwanza: Mwanamke ana hedhi yenye kujulikana kabla ya damu ya ugonjwa. Katika hali hii atatendea kazi hedhi yake na hukumu zake. Ile damu yenye kuzidi ni damu ya ugonjwa ambayo itatendewa kazi kutokana na hukumu zake.

Mfano wa hilo mwanamke anapata hedhi zile siku sita za mwanzo wa kila mwezi. Kisha baada ya hapo akapata damu ya ugonjwa yenye kuendelea. Katika hali hii hedhi yake ni zile siku sita za mwanzo wa kila mwezi na ile nyingine yote ni damu ya ugonjwa. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Faatwimah bint Abiy Hubaysh alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Mimi ni mwanamke nisiyetwaharika. Je, niache kuswali?” Akasema: “Hapana. Huo ni mshipa na wala si hedhi. Pale hedhi yako inapokuja basi acha swalah. Wakati inapomalizika jitwaharishe kisha swali.”[1]

Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia Himnah bint Jahsh:

“Kaa kiasi cha hedhi inavyokuzuia. Kisha baada ya hapo oga na uswali.”[2]

Kutokana na hili mwanamke ambaye yuko na damu ya ugonjwa na ana hedhi yenye kujulikana atakaa kiasi cha hedhi inavyomzuia. Baada ya hapo ataoga na kuswali na kupuuza damu inayotoka.

[1] al-Bukhaariy (306).

[2] Muslim (334).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016