17. Dalili ya kumi na tano kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

15- Nilimsomea Ahmad bin Ahmad bin Muhammad bin Muhammad bin Hamdiy: al-Qaadhwiy Abul-Husayn amekukhabarisheni: Abu Bakr al-Khatwiyb ametuhadithia: Abu ´Umar al-Haashimiy ametuhadithia: Abu ´Aliy al-Lu’lu-iy ametuhadithia: Abu Daawuud as-Sijistaaniy ametuhadithia: Muhammad bin as-Sabbaah ametuhadithia: al-Waliyd bin Abiy Thawr ametuhadithia, kutoka kwa Simaak, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umayrah, kutoka kwa al-Ahnaf bin Qays, kutoka kwa al-´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib aliyesema:

“Nilikuwa Batwhaa´ katika kundi la watu ambalo alikuwemo pia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akatazama mawingu yaliyopita ambapo akasema: “Mnaitaje hii?” Wakasema: “Mawingu.” Akasema: “Vipi mawingu ya mvua?” Wakasema: “Mawingu ya mvua.”Akasema: “Vipi anga?” Wakasema: “Anga.”Akasema: “Hivi mnajua umbali ulioko kati ya mbingu na ardhi?” Wakasema: “Hatujui.”Akasema: “Umbali ulioko kati yake ni miaka 71, 72 au miaka 73. Vivyo hivyo mbingu zilizoko juu yake.” Mpaka alipofikia mbingu ya saba akasema: “Juu ya mbingu ya saba kuna bahari ambayo kufika mpaka chini ni sawa na umbali wa kutoka mbingu moja hadi nyingine. Juu yake kuna mbuzi wanane. Umbali kati visigino na magoti yavyo ni sawa na umbali wa kutoka mbingu moja hadi nyingine. Migongoni mwao ndiko kuna ´Arshi ambapo kutokea chini yake mpaka juu yake ni sawa na umbali wa kutoka mbingu moja hadi nyingine. Allaah (Ta´ala) yuko juu yake.”[1]

[1] Ahmad (1/206), Abu Daawuud (4723), at-Tirmidhiy (3320) ambaye amesema ni nzuri na Swahiyh, Ibn Maajah (193), Ibn Khuzaymah katika ”at-Tawhiyd”, uk. 100-102, Ibn Abiy ´Aaswim (577) na ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 19. Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-ul-Qayyim katika ”Ijtimaa´-ul-Juyuush al-Islaamiyyah”, uk. 87, na dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwilaal-ul-Jannah” (577).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 95
  • Imechapishwa: 02/06/2018