17. Ahl-ul-Bid´ah tu ndio wenye kuudhika na Qur-aan na Sunnah

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

“Haijalishi kitu hata kama kuna ambao hawawezi kuzisikia au kuchukulia kwa ubaya kuzisikiza.”

Bi maana watu wa batili wasioweza kuzisikia. Watu wa haki wanazikubali kwa furaha.

Imaam Ahmad amesema:

“Lililo juu yake ni kuziamini… “

Alisema hivo wakati ilipodhihiri fitina na watu wakaanza kupinga kuonekana kwa Allaah na kuudhika. Kuna mwenye kuudhika na Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) au Aayah ya Qur-aan kuhusu Kuonekana? Hapana. Hakuna ambaye hawezi kuzisikia isipokuwa watu wa batili. Ndio maana amesema hivo.

Imaam Ahmad amesema:

“… na asirudishe herufi hata moja kwenye Hadiyth hizo au nyenginezo zilizopokelewa kutoka kwa wapokezi waaminifu.”

Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazungumzi kwa matamanio yake. Hazungumzi isipokuwa haki. ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Nilikuwa nikiandika kila ninachokisikia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili nikihifadhi. Quraysh wakanizuia na kusema: “Unaandika kila kitu wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwanaadamu ambaye anazungumza katika hali ya hasira na furaha?” Nikaacha kuandika na kumwambia hayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye aliashiria kwenye mdomo na kusema: “Andika! Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko Mikononi Mwake hakuna kinachotoka humo isipokuwa ni haki.”[1]

[1] Abu Daawuud (3647), Ahmad (2/162) na al-Haakim (1/187). Ahmad Shaakir amesema: ”Mlolongo wa wapokezi wake ni Swahiyh.”

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Usuwl-is-Sunnah, uk. 381-382
  • Imechapishwa: 06/08/2017