169. Ni vipi atakaa eda mwanamke mwajiriwa?


Swali 169: Mwanamke wa Kiislamu na ambaye ameajiriwa akifiwa na mumewe na anaishi katika nchi ambayo haimpi mtu yeyote aliyefiwa na ndugu yake likizo isiyozidi siku tatu. Ni vipi atakaa eda katika hali kama hii? Kwa sababu akiamua kukaa eda ule muda uliowekwa katika Shari´ah basi atafukuzwa kazini. Je, aache ule wajibu wa kidini kwa sababu ya kutafuta maisha[1]?

Jibu: Ni lazima kwake kukaa eda ya ki-Shari´ah na alazimiane na eda ndani ya kile kipindi chote cha eda. Inafaa kwake kutoka muda wa mchana kwa ajili ya kazi yake. Kwa sababu ni miongoni mwa yale mahitaji yake muhimu. Wanazuoni wameeleza kwamba inafaa kwa mwanamke mwenye kukaa eda kwa ajili ya kufiwa na mume wake kutoka mchana kwa ajili ya mahitaji yake. Kazi ni miongoni mwa mahitaji muhimu zaidi. Akihitajia kufanya hivo usiku basi itafaa kwake kutoka kwa ajili ya dharurah kwa kuchelea asije kufukuzwa. Haifichikani yale madhara yanayopelekea kwa yeye kufukuzwa kazini akiwa ni mwenye kuhitaji kazi hii. Wanazuoni wametaja sababu nyingi katika kujuzisha yeye kutoka nje ya nyumba ya mumewe ambayo yeye anawajibika kukaa eda ndani yake. Baadhi ya sababu hizo ni nyepesi ukilinganisha na yeye kutoka kwa ajili ya kazi ikiwa kazi hiyo ni yenye kumlazimu. Msingi wa jambo hilo ni maneno Yake (Subhaanah):

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  amesema:

“Na yale niliyokuamrisheni basi yaendeeni kiasi muwezavyo.”[3]

Kuna maafikiano juu ya usahihi wake.

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (22/201-202).

[2] 64:16

[3] Ahmad (7288) na Muslim (1337).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 126-127
  • Imechapishwa: 31/01/2022