164. Kama aliacha wasia pengine akasalimika na adhabu

Swali 164: Je, anaadhibiwa maiti endapo atausia asifanyiwe maombolezo kisha akafanyiwa maombolezo[1]?

Jibu: Allaah ndiye anajua zaidi. Ni lazima kwao kutahadhari. Pengine atakuwa mwenye kusalimika ikiwa aliwausia na akawatadharisha kwa kujengea kanuni ya ki-Shari´ah iliyochukuliwa kutoka katika Aayah ya Qur-aan:

وَلَا تَزِرُ وَازِرَةٌ وِزْرَ أُخْرَىٰ

“Wala habebi mbebaji mzigo [wa dhambi] wa mtu mwengine.”[2]

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/415-416).

[2] 06:164

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 120
  • Imechapishwa: 02/02/2022