162. Kushukuru ni lazima wakati wa msiba?


Swali 162: Je, ni lazima kushukuru wakati wa msiba[1]?

Jibu: Kilicho cha lazima ni kusubiri. Kuhusu kuridhia na kushukuru ni mambo yamependekezwa. Kuna mambo matatu wakati wa msiba:

1 – Subira. Nayo ni lazima.

2 – Kuridhia. Imependekezwa.

3 – Kushukuru. Ndio bora zaidi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/413).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 118
  • Imechapishwa: 28/01/2022