Swali 160: Sisi kazini kwetu anapofariki mfanyakazi mwenzetu basi kunasambazwa karatasi inayoonyesha ni wapi ataswaliwa au mahali pa tanzia. Ni ipi hukumu[1]?
Jibu: Sitambui ubaya wowote wa kufanya hivo. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya juu ya an-Najaashiy. Hakuna ubaya wa kusema kuwa watamswalia katika msikiti fulani.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/410).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 117
- Imechapishwa: 22/01/2022