4 – Mwanamke mwenye hedhi analazimika kuoga wakati inapoisha hedhi yake. Atafanya hivo kwa kutumia maji kwa nia ya kujisafisha mwili wake wote. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Itapokujia hedhi yako basi wacha swalah na itapoondoka basi oga na uswali.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

Namna yake mwanamke atanuia kuondosha hadathi au kujitwahirisha kwa ajili ya kuswali na mfano wake kisha atasema:

بسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

halafu atamimina maji juu ya mwili wake wote[1] na ataingiza maji kwenye mashina ya nywele za kichwani mwake. Hahitajii kuzifumua nywele zake ikiwa zimesukwa. Isipokuwa tu ataziingiza maji. Ni vizuri akitumia mkunazi au vifaa vinavyosafisha pamoja na maji. Imependekezwa kuchukua pamba ilio na miski au kitu kingine katika manukato na akaiingiza ndani ya tupu yake baada ya kuoga. Alimwamrisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Asmaa´ kufanya hivo[2].

[1] Baada ya kujisafisha tupu yake kwa maji na akatawadha.

[2] Muslim.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 28/10/2019