16. Watu hawa kazi yao ni kulipua, migomo na maandamano

Ameandika kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Haijuzu kwa mtu mwingine kusimamisha adhabu za Kishari´ah isipokuwa yule mtawala wa waislamu. Pindi kwa masikitiko itapodhihiri kwamba hakuna ambaye anasimamisha adhabu za Kishari´ah, haina maana kwamba mlango wa Kishari´ah hautakiwi kufunguliwa. Lakini hilo linatakiwa kutukumbusha kuwajuza waislamu wote juu ya kutokuwepo nchi ya Kiislamu inayosimamisha adhabu za Kishari´ah isipokuwa tu ambayo inatendea kazi hukumu zote za Kishari´ah. Wakati tutapoyakumbuka haya, basi ni wajibu kufanya bidii kusimamisha nchi hii ya Kiislamu. Kama mnavyojua husema siku zote kwamba hayo hayawezi kupatikana kwa fujo, hamasa na kelele, isipokuwa ni kwa kupambana.”[1]

Mosi amesema:

“Haijuzu kwa mtu mwingine kusimamisha adhabu za Kishari´ah isipokuwa yule mtawala wa waislamu.”

Kuhusu hayo kuna maafikiano juu ya waungwana na tofauti juu ya watumwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Pindi wajakazi wenu watapofanya uzinzi na ukabaini uzinzi wao, basi wachapeni bakora na wala msiwakebehi kwa dhambi yao. Watapofanya uzinzi tena, wachapeni bakora na wala msiwakebehi kwa dhambi yao. Watapofanya uzinzi kwa mara ya tatu na ukabaini uzinzi wao, basi wauzeni japokuwa kwa thamani ya kamba.”[2]

Pili amesema:

“Pindi kwa masikitiko itapodhihiri kwamba hakuna ambaye anasimamisha adhabu za Kishari´ah, haina maana kwamba mlango wa Kishari´ah hautakiwi kufunguliwa. Lakini hilo linatakiwa kutukumbusha kuwajuza waislamu wote juu ya kutokuwepo nchi ya Kiislamu inayosimamisha adhabu za Kishari´ah isipokuwa tu ambayo inatendea kazi hukumu zote za Kishari´ah.”

Ilitakikana kwa Shaykh kufanya uvuaji juu ya Saudi Arabia (ambayo ndio nchi pekee inayosimamisha adhabu zilizowekwa katika Shari´ah) ili kuzuia uvumizi wa watu wabaya.

Tatu ni kwamba maneno yake yanatakiwa kufasiriwa kwamba anakusudia nchi yake. Maneno ya muislamu yanatakiwa kufasiriwa kwa uzuri iwezekanavyo.

Nne amesema:

“Pindi kutapodhihiri masikitiko kwamba hakuna ambaye anasimamisha adhabu za Kishari´ah.”

Hayo yasitupelekee kufanya mambo ambayo hayakubaliki Kishari´ah, kama vile mapinduzi, migomo, maandamano, mauaji ya kuvizia na kujilipua mambo ambayo yanaharibu na kuteketeza mali, watu na mimea. Mambo kama haya hayafanywi na waislamu ambao wanamcha Allaah (´Azza wa Jall); mambo haya yanafanywa na watu wa matamanio yaliyojengwa juu ya ujinga, watu wa Bid´ah na upotevu kutoka kwa watu wa mapinduzi Hizbiyyuun na Takfiyriyyuun.

[1] Uk. 11

[2] al-Bukhaariy (6839) na Muslim (1703).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 27/11/2018