Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَلِتُكَبِّرُوا اللَّـهَ عَلَىٰ مَا هَدَاكُمْ

“… na ili mumtukuze Allaah kwa kuwa amekuongozeni.”[1]

Aayah hii ni dalili inayofahamisha kuwa ni jambo limewekwa katika Shari´ah kufanya Takbiyr katika usiku wa ´Iyd na ile siku ya ´Iyd. Wanachuoni wanatumia Aayah hii, na Hadiyth na mapokezi mengine, kuonyesha kuwa ni jambo limesuniwa kufanya Takbiyr usiku wa ´Iyd na mchana wake.

Aayah inaashiria ya kwamba Mungu wa haki na mwabudiwa ni mkubwa na mtukufu. Allaah ni mkubwa kuliko kila kitu. Allaah (Ta´ala) amesema:

قُلْ أَيُّ شَيْءٍ أَكْبَرُ شَهَادَةً ۖ قُلِ اللَّـهُ

“Sema: “Ni kitu gani ushahidi wake ndio mkubwa zaidi?” Sema: “Allaah.”[2]

[1] 02:185

[2] 06:19

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 28
  • Imechapishwa: 02/06/2017