Damu ya ugonjwa ina maana ya damu yenye kuendelea kwa mwanamke kwa njia ya kwamba haikatiki kamwe au inakatika kwa muda mfupi kama mfano wa siku moja au mbili kwa mwezi.

Dalili ya hali ya kwanza ambapo damu haikatiki kamwe imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

“Faatwimah bint Abiy Hubaysh alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumwambia: “Ee Mtume wa Allaah! Mimi ni mwanamke nisiyetwaharika. Je, niache kuswali?” Akasema: “Hapana. Huo ni mshipa na wala si hedhi. Pale hedhi yako inapokuja basi acha swalah. Wakati inapomalizika jitwaharishe kisha swali.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Mimi ni mwanamke mwenye damu ya ugonjwa na sitwahariki…”[2]

Dalili ya hali ya pili ambapo damu inakatika kwa muda mfupi ni Hadiyth ya Himnah bint Jahsh (Radhiya Allaahu ´anhaa) wakati alipokuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

“Ee Mtume wa Allaah! Mimi nina damu ya ugonjwa kubwa na yenye nguvu.”[3]

Ameipokea Ahmad, Abu Daawuud na at-Tirmidhiy ambaye amesema kuwa ni Swahiyh. Imenukuliwa kuwa Imaam Ahmad anaonelea kuwa ni Swahiyh wakati al-Bukhaariy anaonelea kuwa ni nzuri.

[1] al-Bukhaariy (306).

[2] al-Bukhaariy (325).

[3] Abu Daawuud (287), at-Tirmidhiy (128) na Ahmad (67381-382).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016