16. Sifa ya tano ya mwanamke ili aweze kuitengeneza jamii

Sifa ya tano: Uchangamfu katika kulingania.

Mwanamke anatakiwa kuwa na jukumu la kuwaelemisha wasichana wa jinsia yake. Hilo linakuwa kupitia jamii. Ni mamoja anafanya hivo katika masomo, sekondari au chuo kikuu au ngazi mbali mbali zilizo chini ya hapo. Kadhalika anaweza kufanya hivo kupitia jamii baina ya wanawake katika yale matembezi ambayo kunapatikana ndani yake ukumbusho wenye faida.

Tumefikiwa na khabari ya kwamba kuna wanawake walio na kazi kubwa katika masuala haya na kwamba wamepanga vikao vya wanawake wa jinsia yao juu ya kuelimishana elimu ya dini. Hili bila ya shaka ni jambo zuri ambalo mwanamke anasifiwa kwalo. Ni thawabu anazojihifadhia baada ya kufa kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake yote hukatika isipokuwa vitu vitatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea.”

Mwanamke akiwa na uchangamfu wa kueneza Da´wah kupitia matembezi, kati ya jamii kama masomo na kwenginepo, basi anakuwa na athari kubwa na kazi kubwa katika kuitengeneza jamii.

Haya ndio ninayoweza kukumbuka hivi sasa kuhusiana na jukumu alilonalo mwanamke katika kuitengeneza jamii na sababu tulizotaja zinazofanya kuyafikia malengo hayo.

Ninamuomba Allaah atufanye kuwa ni waongofu, wenye kuongoza, wema na atutunukie huruma Yake – hakika Yeye ndiye Mwingi wa kutoa. Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengi. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah wake na wale watakaowafuata kwa wema mpaka siku ya mwisho.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017