Ramadhaan ilifaradhishwa mwaka wa pili baada ya kuhajiri ambapo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafunga miaka tisa. Kufunga kulipitia hatua mbili:

1- Hatua ya kwanza mtu alikuwa na chaguo kati ya kufunga na kulisha pamoja na kwamba kufunga ndio ilikuwa bora zaidi.

2- Hatua ya pili ilikuwa ulazima wa kufunga bila ya mtu kuwa na chaguo. al-Bukhaariy na Muslim wamepotea kupitia kwa Salamah non al-Akwaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba kulipoteremka:

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ

“Na ni juu ya wale wanaoiweza [kufunga swawm] lakini kwa tabu watoe fidia kulisha masikini.”

Alikuwa anayetaka kula na kutoa fidia anafanya hivo. Hali iliendelea hivo mpaka kuliposhuka Aayah iliobaada yake ambapo ikaifuta. Nayo ni maneno Yake (Ta´ala):

فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Basi atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi [mpya] na afunge  swawm. Na atakayekuwa mgonjwa au safarini basi [atimize] idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Hapo ndipo Allaah akatuwajibishia kufunga bila ya kuwa na chaguo jengine.

Hailazimiki kufunga mpaka kuthibiti kuingia kwa mwezi. Mtu asifunge kabla ya kuingia kwa mwezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wetu asiitangulizie Ramadhaan kwa kufunga siku moja au siku mbili; isipokuwa mtu ambaye alikuwa na mazowea ya kufunga basi aendelee kufunga siku hiyo.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

[1] 02:183

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 19-21
  • Imechapishwa: 10/04/2020