16. Ni ipi hukumu ya kutafuna ubani na tubaku wakati wa kufunga?


Swali 16: Ni ipi hukumu ya kutafuna ubani na tubaku wakati wa kufunga?

Jibu: Haina shaka kuwa tubaku na sigara kunaharibu swawm. Kuhusu ubani, wanachuoni wametofautiana juu yake. Baadhi wanaonelea kuwa ni wajibu au ni bora kuiepuka. Wengine wanajuzisha hilo. Ubani unaokusanya mate unatakiwa kuepukwa. Sisemi kuwa ubani unaharibu swawm, isipokuwa imechukizwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaas-Swiyaam, uk. 32
  • Imechapishwa: 12/06/2017