Ama kuhusiana na mashairi, yana nafasi ya haki za wanandoa nyumbani wakati wanandoa wamekaa pamoja katika jahazi ya maisha. Maisha ni bahari inayopigwa na mawimbi na dhoruba. Yana nyakati zinazofurahisha kama jinsi yana nyakati zinazosikitisha. Yana kukasirika na kuridhia. Ndio maana wafanyakazi wa safina hii wanahitajia ushirikiano na kuandaa vifaa vyenye kusalimisha uhai ili wanandoa waweze kupita juu ya bahari kwa raha, furaha na amani na kufika nchikavu Aakhirah ambapo namuomba Allaah (´Azza wa Jall) iwe ni Pepo. Huko wanandoa watakusanyika kama jinsi walivyokusanyika duniani. Katika safari hii ya maisha haya wanandoa wanahitajia kujua haki baina yao. Haki za wanandoa katika Uislamu zimejengwa juu ya kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wakati mtu anapotekeleza haki hizi anatarajia thawabu kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 24-25
  • Imechapishwa: 24/03/2017