al-Halabiy amesema:

“5- Kuhusiana na Shu´bah na al-A´mash, Shaykh Rabiy´ al-Madkhaliy amekiri kuwa walitumbukia kwenye Bid´ah. Alisema katika “Mujaazafaat al-Haddaad”:

“3- Amesema (Mahmuud al-Haddaad): “Mwandishi amevunja hilo pindi alipokuwa ananiraddi katika kijitabu ambapo amemfanyia Tabdiy´ Shu´bah na al-A´mash na kumponda Sufyaan ath-Thawriy pamoja na kuwasifu Ahl-ul-Bid´ah.”

Kijitabu hicho bado kipo na sikumponda kabisa Sufyaan ath-Thawriy. Ninamzingia kuwa ni mmoja katika maimamu wakubwa na Allaah peke yake ndiye anajua ni namna gani ninavyompenda na kumtukuza. Hata hivyo upetukaji wa watu hawa umenifanya kunukuu aliyosema ash-Shaafi´iy na wengine juu ya msimamo wa Sufyaan bin Jaabir al-Ju´fiy.””

Mahmuud al-Haddaad ni mtu wa Bid´ah na ni mwongo. Hakuna anayetegemea nukuu zake isipokuwa mwenye kufanana naye. Moja katika dhambi zake ni kitabu alichokiandika kwa mkono wake kwa jina “al-Khamiys”, bi maana jeshi lililopangwa lililo na kituo cha kati, cha nyuma, cha mbele na mbawa. Kitabu hiki kimefikia kurasa 400 zilizoandikwa kwa mkono, ikiwa na maana ya kwamba kingefikia kurasa 1000 lau kingechapishwa. Kitabu hiki kimejaa madhambi na mashambulizi kwa ´Allaamah al-Albaaniy (Rahimahu Allaah). Pamoja na hivyo al-Halabiy siku zote anaonesha kuwa ameshikamana na al-Albaaniy na kila siku utamsikia akisema “Shaykh wetu, Shaykh wetu”, lakini hakufanya lolote.

Kadhalika ´Abdul-Laatwiyf Baashmiyl aliandika kijitabu kilicho jaa uongo na upotoshaji dhidi ya al-Albaaniy na Salafiyyuun ambacho nilikiraddi kwa kijitabu na kufichua uongo wake, usaliti wake na dhuluma zake kwa al-Albaaniy na Salafiyyuun. Pamoja na hivyo al-Halabiy hakufanya lolote.

Hatetei wala kupigana vita isipokuwa inapokuja katika kufanyiwa dhuluma, ujinga na mashambulizi kwa Salafiyyuun na khaswa mimi ambaye nimekuwa ndio lengo lake kwa ajili ya kampeni zake mbaya na mashambulizi yake. Ruduud zake kwa Takfiyriyyuun hazikuwa kwa ajili ya Salafiyyah. Mara nyingi hazikuwa isipokuwa ni kwa sababu ya kibinafsi. Si sawa kusema kuwa ametetea mfumo wa Salaf na Salafiyyuun. Dalili kubwa ya haya niyasemayo ni urafiki wake mkubwa na utetezi wake kwa Takfiyriyyuun na wafuasi zao.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://rabee.net/ar/articles.php?cat=8&id=236
  • Imechapishwa: 08/01/2017