16. Mfano wa kumi na moja kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan


Kama jinsi Allaah alivyowakadhibisha mayahudi na manaswara pindi walipodai kuwa wamemuua na kumsulubu Masihi kila Aayah ya Qur-aan inawakadhibisha Raafidhwah. Allaah (Ta´ala) Amesema:

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ

“Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaoihifadhi.”[1]

Kadhalika wanakadhibishwa na Maswahabah, akiwemo ´Aliy na watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), maafikiano na Ummah mzima wa Kiislamu umekubaliana mashariki na magharibi, kuanzia karne ya kwanza mpaka ya kumi na tano.

Wale wanaodai kuwa Maswahabah wamepotosha, wamepunguza na wameongeza Qur-aan sio katika Ummah wa Kiislamu. ´Aqiydah yao potevu, matendo yao ya kuoza na maneno yao ya uongo juu ya Kitabu cha Allaah na Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanathibitisha ya kwamba sio Waislamu.

Lililo baya zaidi kuliko uongo huu ni yale aliyofanya na kusema an-Nuuriy at-Twabarsiy. Husayn al-Muusaawiy amesema:

“Hakuna andiko lolote linalohitajia kuithibitisha Qur-aan. Lakini vitabu vya wanachuoni wetu na maneno ya Mujtahiduun wetu yanasema wazi kabisa kuwa imepotoshwa na ndio kitabu pekee kilichopotoshwa.”[2]

an-Nuuriy at-Twabarsiy amekusanya kitabu kikubwa ili kuthibitisha kuwa Qur-aan imepotoshwa. Kinaitwa “Fasl-ul-Khitwaab fiy Ithbaati Tahriyfi Kitaabi Rabb-il-Arbaab”. Humo mna zaidi ya mapokezi 2000 yanayosema kuwa Qur-aan imepotoshwa. Amekusanya maneno ya wanachuoni wa Shiy´ah wote juu ya kwamba Qur-aan walionayo leo waislamu imepotoshwa. Amethibitisha kuwa wanachuoni wote wa Shiy´ah, waliotangulia na waliokuja baadae, wanaonelea kuwa Qur-aan ya leo walionayo waislamu imepotoshwa. Nina nuskha moja ya kitabu “Fasl-ul-Khitwaab”. Raafidhwah wakisema kuwa hawaonelei kabisa ya kuwa Maswahabah wameipotosha Qur-aan usiwaamini. Yule mwenye kupinga hilo katika wao anafanya Taqiyyah, kudhihirisha kinyume na anavoamini mtu. Huyu ni shari zaidi kuliko yule asiyepinga hilo. Ni mikono yao michafu ndio ambayo imepotosha, kubadili na kupunguza Qur-aan. Allaah ameahidi kukihifadhi Kitabu Chake. Anafanya waumini wanawafedhehesha na kuonyesha uongo wao na Kitabu Chake kinabaki katika mikono ya waumini kama jinsi kilivyoteremshwa. Hivo ndivyo kitavyobaki mpaka hapo kitaponyanyuliwa.

[1] 15:09

[2] Kashf-ul-Asraar wa Tabri-at-ul-A-immah al-Athaar, uk. 79.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 43-44
  • Imechapishwa: 19/03/2017