16- Madhambi yanawaathiri wanyama


Madhambi yanawaathiri watu wengine na wanyama. Yanapelekea yeye na wengine wakaunguzwa kwa sababu ya madhambi na dhuluma. Abu Hurayrah amesema:

“Tandawala mkubwa[1] inakufa chichani mwake kwa sababu ya dhuluma za mwenye kudhulumu.”

Mujaahid amesema:

“Wanyama wanawalaani wale wanaadamu wenye kutenda madhambi pindi kunakuwa ukame mkubwa na mvua ikaacha kunyesha na wakasema: “Haya ni kwa sababu ya maasi ya wanaadamu.””

´Ikrimah amesema:

“Wanyama wa ardhini mpaka mende na nge wanasema: “Tumenyimwa mvua kwa sababu ya madhambi ya wanaadamu.””

Haitoshi kuadhibiwa kwa sababu ya madhambi yake. Analaaniwa hata na wale wasiokuwa na madhambi.

[1] Tazama https://sw.wikipedia.org/wiki/Tandawala

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 71
  • Imechapishwa: 08/01/2018