16. Kusafika na hedhi na mtiririko mweupe


Swali 16: Masiku ya mwisho ya hedhi na kabla ya kutwahirika mwanamke haoni athari ya damu. Je, afunge siku hiyo ilihali hajaona mtiririko mweupe?

Jibu: Ikiwa mazowea yake haoni mtiririko mweupe, kama ilivyo kwa baadhi ya wanawake, basi atatakiwa kufunga. Na ikiwa amezowea kuona mtiririko mweupe, basi asifunge mpaka kwanza aone mtiririko mweupe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 60 su-aal wa jawaab fiy Ahkaam-il-Haydhw, uk. 16-17
  • Imechapishwa: 25/06/2021