16. Kuoanisha kati ya ujuu wa Allaah na kushuka Kwake katika mbingu ya dunia


Ujuu wa Allaah (Ta´ala) ni katika sifa za kidhati ambayo katu haiachani Naye. Pamoja na hivyo ni jambo halipingani na kushuka Kwake katika mbingu ya dunia. Sifa hizi mbili zinaoanishwa ifautavyo:

Mosi: Maandiko katika Qur-aan na Sunnah imeyaoanisha na hayawezi kutaja kitu kisichowezekana kabisa kama tulivyotangulia kusema.

Pili: Hakuna kitu ambacho ni mfano wa Allaah kwa njia yoyote ile. Kuteremka Kwake sio kama wanavyoteremka viumbe mpaka mtu aseme kuwa kunapingana na ujuu Wake – na Allaah ndiye anajua zaidi.