16. Kuoanisha kati ya ujuu wa Allaah na kushuka Kwake katika mbingu ya chini

Ujuu wa Allaah (Ta´ala) ni katika sifa za kidhati ambayo katu haitengani Naye. Pamoja na hivyo ni jambo halipingani na kushuka Kwake katika mbingu ya chini. Sifa hizi mbili zinaoanishwa ifautavyo:

1- Maandiko katika Qur-aan na Sunnah imeyaoanisha na hayawezi kutaja kitu kisichowezekana kabisa kama tulivyotangulia kusema.

2- Hakuna kitu ambacho ni mfano wa Allaah katikaa sifa Zake zote. Kuteremka Kwake sio kama wanavoshuka viumbe mpaka mtu aseme kuwa kunapingana na ujuu Wake – na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fath Rabb-il-Bariyyah, uk. 55
  • Imechapishwa: 28/04/2020